Monday, August 26, 2013

TAREHE YA KUANZA KWA ODEX

Tunapenda kuwakumbusha wanafunzi wote wa OUT mliojiandikisha kufanya mitihani maalum kwa wahitaji (ODEX) kuwa mitihani hiyo itaanza Jumatatu ijayo, tarehe 2 August 2013 na kumalizika Alhamisi, tarehe 5 August 2013.
Tunawatakia mtihani mwema.

TATIZO LA KIUFUNDI

Tunapenda kuwaomba radhi wasomaji wetu wa blog yetu hii kwa kutopata taarifa kwa muda mrefu kidogo. Hii imetokana na matatizo ya kiufundi yaliyokuwa juu ya uwezo wetu. Hata hivyo, matatizo hayo yameshatatuliwa. Hivyo tutaendelea kuwapatia taarifa mbalimbali zinazohusu OUT kituo cha Tanga na nyinginezo kwa ujumla. Ahsanteni!

Sunday, August 4, 2013

MATOKEO YA MITIHANI YA JUNE 2013

Tunapenda kuwajulisha wanafunzi wote wa OUT kuwa matokeo ya mitihani iliyofanyika June 2013 yatakuwa tayari kwenye SARIS zenu kufikia tarehe 12 August 2013.
Wasalaam!