Ndugu wahitimu watarajiwa wa OUT 2013,
tunapenda kuwajulisha kuwa chuo kimeongeza muda wa kukamilisha malipo ya ada zinazodaiwa kwa wanafunzi wanaotarajia kuhitimu mwaka huu 2013. Tarehe ya mwisho itakuwa ni 20/09/2013.
Hivyo, mnashauriwa kukamilisha madeni yetu kabla ya muda huo kupita, ama sivyo hamtaruhusia kuhitimu mwaka huu, badala yake itawabidi kusubiri mpaka mwaka unaofuata.
Nawatakia maandalizi mema.