Wednesday, October 30, 2013

UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MASOMO 2013/2014 NA SHEREHE YA KUWAPONGEZA WAHITIMU WA OUT-TANGA 2013

Kwa wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kituoo cha mkoa wa Tanga,
Tunapenda kuwafahamisha kuwa shughuli za ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo 2013/2014 utafanyia Jumamosi na Jumapili, tarehe 2 na 3 Novemba 2013 katika eneo la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania-kituo cha Tanga.
Halikadhalika, shughuli hizo za ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo (orientation) zitaambatana na sherehe za kuwapongeza wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania walioko mkoani Tanga. Sherehe hizo zitaanza kwa maandamano yatakayoanzia barabara ya 20 (CCM Hall) saa 1.30 asubuhi na kupokelewa na mgeni rasmi katika eneo la Chuo lililopo Chumbageni.
Hivyo, wanachuo wote, wapya na wanaoendelea, mnahitajika kuhudhuria matukio hayo muhimu bila kukosa kwa siku zote mbili.
Karibuni sana.