Tuesday, April 16, 2013

USAJILI WA WANAFUNZI WALIOZIDISHA MIAKA 8 YA MASOMO

Chuo kikuu huria cha Tanzania kinawatangazia wanafunzi wote waliozidisha miaka 8 ya masomo (wenye namba za usajili ...../T.04 kurudi nyuma) kuwa chuo kinadhamiria kuwafutia usajili wao wa masomo kutokana na kuzidisha muda unaokubalika kisheria.
Hivyo, yeyote anayehusika anahitajika kumuandikia barua DVC (Academic)  akieleza sababu zilizomfanya azidishe muda na kuomba kuongezewa muda wa kukamilisha masomo. Barua hizo zipitie kwa Mkurugenzi wa kituo (DRC), na ziambatanishwe na nakala ya SARIS ya mwanafunzi husika pamoja na ushahidi wa sababu atakazozieleza. Mwisho wa kuandika barua hizo ni tarehe 19 June 2013. Kwa kushindwa kufanya hivyo, mwanafunzi husika atakuwa amejifuta chuo mwenyewe. OUT Tanga Centre inawatkia utekelezaji mwema wa agizo hilo.

No comments:

Post a Comment