Uongozi, wahadhiri pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania-kituo cha Tanga, tunapenda kuwashukuru wanafunzi wote walioshiriki katika shughuli za kufungua mwaka mpya wa masomo 2013/2014 pamoja na sherehe za kuwapongeza wahitimu wa mwaka huu. Ushirikiano wenu ndio ambao kwa kiasi kikubwa ulizifanya shughuli hizo kufana.
Aidha, tunawaomba radhi kwa mapungufu yoyote yaliyojitokeza. Karibuni sana.
No comments:
Post a Comment