Wednesday, December 4, 2013

TANZIA

Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kituo cha Tanga unasikitika kuwatangazia wanajumuia wote wa OUT kuwa mwanachuo Sarah Ayoub, ambaye alikuwa akisoma kozi ya Sheria (LLB) mwaka wa tatu amefariki dunia siku ya Ijumaa, tarehe 29 Novemba 2013 na kuzikwa siku ya Jumapili, tarehe 1 Desemba 2013 jijini Dar es Salaam.
Kifo cha marehemu kilisababishwa na matatizo ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa karibia mwaka mzima.
Marehemu ameacha mume pamoja na watoto wawili.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina!
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe!

No comments:

Post a Comment