Wednesday, December 4, 2013

EXTENSSION OF TIME FOR COURSE REGISTRATION!

OUT management would like to inform you that the time for course registration has been extended to 16th December 2013.
All students who have not yet registered their courses are therefore required to accomplish their registration before the 16th since there will be no extenssion any more.
Thanks.

TANZIA

Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kituo cha Tanga unasikitika kuwatangazia wanajumuia wote wa OUT kuwa mwanachuo Sarah Ayoub, ambaye alikuwa akisoma kozi ya Sheria (LLB) mwaka wa tatu amefariki dunia siku ya Ijumaa, tarehe 29 Novemba 2013 na kuzikwa siku ya Jumapili, tarehe 1 Desemba 2013 jijini Dar es Salaam.
Kifo cha marehemu kilisababishwa na matatizo ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa karibia mwaka mzima.
Marehemu ameacha mume pamoja na watoto wawili.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina!
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe!

Monday, November 25, 2013

DEADLINE FOR COURSE REGISTRATION!

We would like to remind again all OUT students that the deadline for course registration is on 30th November 2013.
Only 4 days left, so make sure that you register your courses before that day.
Thanks.

Sunday, November 17, 2013

COURSE REGISTRATION

We would like to remind you, OUT students, to complete the exercise of retistering the courses that you intend to undertake for this academic year 2013/2014 before the 30th November 2013.
NOTE: You are required to register only new courses that you have never yet registered before.
Thanks.

Monday, November 4, 2013

SHUKRANI!

Uongozi, wahadhiri pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania-kituo cha Tanga, tunapenda kuwashukuru wanafunzi wote walioshiriki katika shughuli za kufungua mwaka mpya wa masomo 2013/2014 pamoja na sherehe za kuwapongeza wahitimu wa mwaka huu. Ushirikiano wenu ndio ambao kwa kiasi kikubwa ulizifanya shughuli hizo kufana.
Aidha, tunawaomba radhi kwa mapungufu yoyote yaliyojitokeza. Karibuni sana.

RUHUSA YA KUSOMA MASOMO 2 YA KUFUNDISHIA KWA WANAFUNZI WA B.ED

Tunapenda kuwajulisha wanafunzi wanaosoma B.ED waliojiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 na 2012/2013 kuwa nao wanaruhusiwa kusoma masomo mawili ya kufundishia (teaching subjects) kwa kufuata muongozo wa wanafunzi wapya wa B.Ed wa mwaka huu mpya wa masomo 2013/2014 kama inavyojionesha katika Prospectors ya mwaka huu 2013/2014.
Kwa atakayependa kusoma masomo hayo 2 ya kufundishia, atahitajika kusoma units 12 kwa somo kuu (major) na units 6 kwa somo la pili (minor).
ZINGATIA:
Suala hili ni la hiyari kwa wanafunzi wa 2011/2012 na 2012/2013, lakini ni la lazima kwa wanafunzi wapya wa B.Ed wa mwaka huu wa masomo 2013/2014.
Tunawatia ufanisi mwema katika masomo yenu.

Wednesday, October 30, 2013

UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MASOMO 2013/2014 NA SHEREHE YA KUWAPONGEZA WAHITIMU WA OUT-TANGA 2013

Kwa wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kituoo cha mkoa wa Tanga,
Tunapenda kuwafahamisha kuwa shughuli za ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo 2013/2014 utafanyia Jumamosi na Jumapili, tarehe 2 na 3 Novemba 2013 katika eneo la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania-kituo cha Tanga.
Halikadhalika, shughuli hizo za ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo (orientation) zitaambatana na sherehe za kuwapongeza wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania walioko mkoani Tanga. Sherehe hizo zitaanza kwa maandamano yatakayoanzia barabara ya 20 (CCM Hall) saa 1.30 asubuhi na kupokelewa na mgeni rasmi katika eneo la Chuo lililopo Chumbageni.
Hivyo, wanachuo wote, wapya na wanaoendelea, mnahitajika kuhudhuria matukio hayo muhimu bila kukosa kwa siku zote mbili.
Karibuni sana.

Wednesday, September 4, 2013

MWISHO WA KULIPA ADA KWA WAHITIMU WA OUT 2013

Ndugu wahitimu watarajiwa wa OUT 2013,
tunapenda kuwajulisha kuwa chuo kimeongeza muda wa kukamilisha malipo ya ada zinazodaiwa kwa wanafunzi wanaotarajia kuhitimu mwaka huu 2013. Tarehe ya mwisho itakuwa ni 20/09/2013.
Hivyo, mnashauriwa kukamilisha madeni yetu kabla ya muda huo kupita, ama sivyo hamtaruhusia kuhitimu mwaka huu, badala yake itawabidi kusubiri mpaka mwaka unaofuata.
Nawatakia maandalizi mema.

Monday, August 26, 2013

TAREHE YA KUANZA KWA ODEX

Tunapenda kuwakumbusha wanafunzi wote wa OUT mliojiandikisha kufanya mitihani maalum kwa wahitaji (ODEX) kuwa mitihani hiyo itaanza Jumatatu ijayo, tarehe 2 August 2013 na kumalizika Alhamisi, tarehe 5 August 2013.
Tunawatakia mtihani mwema.

TATIZO LA KIUFUNDI

Tunapenda kuwaomba radhi wasomaji wetu wa blog yetu hii kwa kutopata taarifa kwa muda mrefu kidogo. Hii imetokana na matatizo ya kiufundi yaliyokuwa juu ya uwezo wetu. Hata hivyo, matatizo hayo yameshatatuliwa. Hivyo tutaendelea kuwapatia taarifa mbalimbali zinazohusu OUT kituo cha Tanga na nyinginezo kwa ujumla. Ahsanteni!

Sunday, August 4, 2013

MATOKEO YA MITIHANI YA JUNE 2013

Tunapenda kuwajulisha wanafunzi wote wa OUT kuwa matokeo ya mitihani iliyofanyika June 2013 yatakuwa tayari kwenye SARIS zenu kufikia tarehe 12 August 2013.
Wasalaam!

Thursday, June 6, 2013

KIPINDI MAALUM TBC!

Mnajulishwa kuwa leo, siku ya Alhamisi, terehe 06/06/2013 kutakuwa na mahojiano maalum yatakayouhusisha uongozi wa juu wa chuo (OUT) katika kipindi cha TUAMBIE kitakachorushwa moja kwa moja katika Televisheni ya TBC1 kuanzia saa 3 kamili usiku. Hivyo, mnakaribishwa nyote kutazama kipindi hicho ili kufahamu mambo mbalimbali yanayokihusu chuo. Tafadhali mjulishe na mwenzako.

Wednesday, June 5, 2013

JUNE 2013 EXAMINATION!




Get to know that the June 2013 Examination session has already started from Monday, the 3rd of June.
The OUT students are therefore busy sitting for their examinations while others are busy doing final preparations as can be viewed in the uploaded pictures taken from Tanga Regional Centre.

Monday, April 22, 2013

ZAYA MUDA WA KUJISAJILI KWA MITIHANI

Tunapenda kuwajulisha wanafunzi wote wa OUT kuwa tarehe ya mwisho ya kujisajili kwa mitihani ya June 2013 imesogezwa mbele mpaka tarehe 5 May 2013. Kutokana na kuwa tarehe hiyo itaangukia siku ya Jumapili, tunawashauri mkamilishe malipo husika kabla ya Ijumaa ya tarehe 3 May 2013 (ambayo ni siku ya kazi) ili  tuweze kuingiza taarifa za malipo yenu kwenye akaunti zenu za SARIS, na hivyo kuweza kuruhusiwa kujisajili. Tafadhali zingaia.

Tuesday, April 16, 2013

USAJILI WA WANAFUNZI WALIOZIDISHA MIAKA 8 YA MASOMO

Chuo kikuu huria cha Tanzania kinawatangazia wanafunzi wote waliozidisha miaka 8 ya masomo (wenye namba za usajili ...../T.04 kurudi nyuma) kuwa chuo kinadhamiria kuwafutia usajili wao wa masomo kutokana na kuzidisha muda unaokubalika kisheria.
Hivyo, yeyote anayehusika anahitajika kumuandikia barua DVC (Academic)  akieleza sababu zilizomfanya azidishe muda na kuomba kuongezewa muda wa kukamilisha masomo. Barua hizo zipitie kwa Mkurugenzi wa kituo (DRC), na ziambatanishwe na nakala ya SARIS ya mwanafunzi husika pamoja na ushahidi wa sababu atakazozieleza. Mwisho wa kuandika barua hizo ni tarehe 19 June 2013. Kwa kushindwa kufanya hivyo, mwanafunzi husika atakuwa amejifuta chuo mwenyewe. OUT Tanga Centre inawatkia utekelezaji mwema wa agizo hilo.

Monday, April 15, 2013

MWISHO WA USAJILI WA MITIHANI YA JUNE 2013

Wanafunzi wote mnakumbushwa kuwa tarehe ya mwisho ya usajili wa masomo, ulipaji ada na usajili wa mitihani ya June 2013 imekaribia. Hivyo, kamilisha malipo yako ya ada na usajili wa kozi pamoja na mitihani mapema ili kuepuka msongamano katika siku ya mwisho. Mwisho  ni Jumamosi ya tarehe 20/04/2013.  OUT Tanga Centre inakutakia uwajibikaji mwema.

Monday, April 8, 2013

TAREHE YA MWISHO YA FACE-TO-FACE

Wanafunzi wote wa OUT Tanga mnakumbushwa kuwa siku ya mwisho ya kufanya Portfolio Assessment ni Alhamisi, tarehe 11 April 2013. Hivyo, hakikisha kuwa unapata assessment kabla ya muda huo kuisha. Itakuwa ni vigumu kufanya assessment yoyote baada ya tarehe hiyo kutokana na walimu kukabiliwa na majukumu mengine.
Zingatia.

Wednesday, April 3, 2013

COMMENCEMENT OF FACE-TO-FACE WEEK!

To all OUT students (Tanga),
We once again remind you that face-to-face week is going to begin next Saturday, on 6th April 2013. So, each of you (students) is required to attend the first day as there will be some important information to be announced. We wish you good journey to the centre, and happy belated Easter.

Wednesday, March 20, 2013

SELECTED SCHOOLS FOR TEACHING PRACTICE IN TANGA.

To all OUT Tanga students,Following are the schools that have been selected for conducting Teaching Pratcite that begins on 22nd April to 24th May 2013. Old Tanga, Usagara, Chumbageni and Costal secondary schools (at Tanga); Shambalai or Hubiri secondary schools (at Lushoto); Nyerere Memorial secondary school (at Korogwe).

FACE-TO-FACE FOR ACADEMIC YEAR 2012/2013.

To all OUT students of Tanga Regional Centre,You are reminded that face-to-face session for this academic year will be conducted from 6th to 11th April 2013. So, all of you have to get prepared for it.

USAJILI WA MITIHANI YA JUNE 2013.

Usajili wa mitihani (Annuals) pamoja na special Main Timed Tests (MTTs) umeshaanza tangu tarehe 6 March 2013 na utakamilika tarehe 20 April 2013. Hivyo, mnashauriwa kufanya registration mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika siku za mwisho za usajili huo.

KUONGEZWA MUDA WA KULIPA ADA.

Wwanafunzi wote wa OUT mnajulishwa kuwa muda wa kulipa awamu ya pili ya ada ya mwaka wa masomo 2012/2013 umeongezwa. Mwisho wa kulipa ada hizo ni tarehe 20 April 2013

VYETI VYA WAHITIMU WA OUT 2011/2012.

Tunapenda kuwajulisha wahitimu wote wa mwaka wa masomo 2011/2012 kuwa vyeti vipo yatari. Hivyo, kila muhitimu anahitajika kwenda makao makuu ya OUT (Dar es Salaam) akiwa na Academic Transcript.

Thursday, February 28, 2013

MABADILIKO YA TAREHE YA FACE-TO-FACE & TEACHING PRACTICE.

Tunapenda kuwajulisha mabadiliko ya tarehe za Face-To-Face pamoja na Teaching Practice kwa mwaka wa masomo 2012/2013.
Face-to-Face itaanza tarehe 6 mpaka 11 April 2013 kwa wanafunzi wote wa Tanga.
Teaching Practice nayo itaanza tarehe 22 April mpaka 24 May 2013.
Hivho, mnashauriwa kuzingatia mabadiliko haya yaliyosababishwa na kusogezwa mbele kwa tarehe za usahihishaji wa mitihani ya January/February 2013.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokana na mabadiliko haya.

Wednesday, February 27, 2013

STUDENTS PROGRESS POTFOLIO.

To all OUT students-Tanga Regional Centre,
You are informjed that the Students Progress Potfolios are available at the centre.
So, you are reminded to visit the office and collect yours for getting prepared for Face-to-Face.

Wednesday, January 30, 2013

FACE TO FACE SESSION FOR 2012/2013 ACADEMIC YEAR.

To all OUT students - Tanga Regional Centre!
You are informed that face to face session will begin on 16th-21st March 2013.
So, make sure that you fill in your portfolio ready for assessment.
Failure to attend face to face, you will not be allowed to sit for annual examinations that will be conducted in June 2013.
Wishing you all the best.
DRC - Tanga.

Thursday, January 24, 2013

JANUARY/FEBRUARY 2013 EXAMINATIONS!

To all OUT students,
You are reminded that the January/February 2013 Main Timed Tests and Special/Sup Annual Examinations are about to start.
From Monday 28th January to 4th February 2013 there will be Special/Sup Examinations sessions.
Main Timed Tests will be done from 5th-15th February 2013.
The DRC and all OUT Academic and Supporting staff of Tanga Regional Centre wish you all the best in your coming exams.